KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA MAJOHE WAKITOA MAFUNZO KWA WANAVIKOBA WA MAJOHE MAPEMA TAREHE 12 MEI 2022 IKIWA NI MAREJESHO YA MAFUNZO WALIYOPEWA NA TGNP

    Mafunzo hayo yametolewa kwa wanavikoba mbalimbali mnamo tarehe 12 Mei 2022 yakiongozwa na mwalimu wao Bi.Seya baada ya mkutano wake wa vikoba na vikundi takribani 15. 

Bi.Seya ameendelea kuwasisitiza kina mama kuendelea kukopa na kurejesha ili kujenga kipato cha mtu mmoja mmoja hiyvo kupelekea kuongeza kipato cha familia. Hakuishia hapo bali aliwekea mkazo suala la kutenga muda wa kuwa karibu na watoto wao. ili kusaidia  kutambua matatizo wanayokutanan nayo. Pia ameeleza changamoto wanazokutana nazo kina mama katika kurejesha mikopo kutokana na kuachiwa majukumu ya kutunza familia na waume zao ambapo mkopo huo huo hutakiwa kufanyia  biashara na kutoa marejesho. 

Hivyo ameiomba serikali kuwanyoshea mkono wanaume wanaozikimbia familia zao kwa kukimbia majukumu yao na kwa ni sehemu ya ukatili wa kijinsia.

 


Picha ya mwalimu wa vikoba Majohe Bi.Seya akiwa na wanavikundi mbalimbali wa kata ya Majohe wakipewa mafunzo ya ufeminia jinsi na jinsia na wana KC Majohe.

 

Mwezeshaji na mchambuzi wa masuala mbalimbali ya kijinsia Hance Obote kutoka KC Saranga naye aliungana na wanamajohe kutoa elimu ya ufeminia, jinsi na jinsia ikiwa ni katika harakati zake za kutoa mafunzo kwa jamii kutambaua haki zao za msingi na kupinga unyanyasaji wa kujinsia. Amezungumzia somo la jinsi na jinsia kwa kuonyesha utofauti wake na jinsi yanavyoeleweka kwenye jamii. 

Alisema  maana ya jinsi ni kitu ambacho hakubadili kwa maana kimaumbile au katika hali yoyote mfano mwanaume haiwezi kubadilika na kuwa mwanamke hata avishwe mavazi ya kike, lakini jinsia inabadilika kwani ni namna jamii wanavyoishi au  utaratibu wao waliojiwekea wa kuishi au kufanya shughuli zao akatolea mfano jamii ya Kikurya mwanamke akipigwa huamini ndoa  anapendwa na mumewake wakati watu wa pwani wenyewe mwanamke hapigwi anapigwa kwa kanga hivyo jamii imeombwa kubadika kutofanya ukatili kwa namna yoyote ile.

Pia alizungumzia suala la ufeminia kuwa kila mwanamke ni mfeminia na mfeminia hajengwi bali anaongezewa uwezo. Alieleza kuwa kama hupendi kuona mtu akifanyiwa ukatili huo ni ufeminia wa kuzaliwa kinachofanywa na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu ni kumfahamisha mtu haki yake na akinyimwa haki yake afanye nini. Vile vile mtu akifanyiwa ukatili wa aina yoyote hatua gani achukue kudai haki yake. Hivyo amewaomba wanamajohe kutoa taarifa kwenye vyombo husika kama dawati la jinsia, watendaji wa serikali na mashirika mbalimbali ya ketetea usawa wa kijinsia kama TGNP.

 



Mwezeshaji Hance Obote akitoa semina fupi ya ufeminia,jinsi na jinsia kwa wanavikoba wa Majohe vikundi takribani 15.

Mwezeshaji kutoka KC Mabwepande naye ameungana na KC Mjohe kutoa mafunzo kwa wajasiliamali akitoa msisitizo kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia  vinavyofanyika katika jamii na kuwaomba wanajamii taarifa mahali husika huo ndio ufeminia. Pia amewaomba kina mama kuwa na tabia ya kuwakagua watoto wao kwa kuwaogesha ili kujilidhisha kama hawajafanyiwa ukatili na pia kujenga ukaribu  nao  pia kuwasikiliza  watoto wao hii itasaidia kuyajua mengi wanayokutana nayo na kuangalia marafiki  wa karibu wa wanao.

Pia ameonya tabia ya kudhani watu wa karibu kama wazazi, mjomba, shangazi n.k kwamba hawawezi kuwafanyia ukatili watoto wao hivyo  kuamua kuwaachia watototo wao hata kuwaruhusu kulala nao.

 


Picha ya Mwanafeminia na vikundi mbalimbali vya vikoba  Mjohe akitoa mafunzo mafupi ya ufeminia, jinsi na jinsia baada ya makutano yao vikoba jioni nyumbani kwa mwalimu wao wa Vikoba.

Wakati mafunzo yakiendelea alipigiwa simu  na KC Viwege Bi Tatu akieleza ukatili uliojitokeza kwa jirani yake mwanamke akiwa na mama yake mzazi (mgonjwa) alifukuzwa na muwe wake nyumbani na kuambiwa kulala kwenye pagale la nyumba hivo aliomba msaada kwa kiongozi wake ili kuona wanamsaidiaje. Kwa umoja wa wanavikoba walilibeba  tatizo hilo kwa uzito wake na kuamua mapema kesho yake kufika eneo la tukio na kutoa msaada kwa mlengwa. 

Hii imetoa majibu mazuri  kwa mafunzo waliyopata kuwa likijitokeza suala lolote la ukatili taarifa zifike mahali husika ili kutatuliwa  haraka. Aidha wawezeshaji wamewapongeza wanawake hao kwa hatua za haraka walizochukua kumsaidia mwanamke mwenzao.

 


Picha ya kiongozi wa KC Majohe akipokea simu ya ukatili wa kijinsia kwa mkazi wa Viwege wakati mafunzo yakiendelea kutolewa kwa Vikoba vya Majohe.

Baada ya mafunzo kumalizika wachangiaji walionyesha kulielewa somo kwa kutoa ushuhuda wao juu ya unyanyasaji unaendelea katika jamii zao mmoja wa wasemaji akieleza jinsi walivyonyanganywa  mtoto wa miezi mitatu (3) na baba asiyejulikana baada ya kifo cha ndugu yao. Aidha ameendelea kueleza kuwa huyo baba aliyepewa mtoto hakuwahi kutambulishwa na marehemu ndugu yao na hakuwahi kujitokeza hata kipindi cha msiba hakuwepo. Hivyo ilionekana mtoto ana baba wawili baada ya yule aliyetambulishwa na marehemu ndugu yao kama mzazi mwenza akajitokeza mzazi mwingine kudai mtoto.

Waliitwa serikali ya mtaa na watendaji wao kumpatia baba huyo mtoto lakini kama ndugu wa marehemu hawakuridhishwa na maamuzi ya watendaji hao waliendelea kutia ugumu mwisho wake walinyanganywa kwa nguvu, mpaka sasa mwezi mmoja (1) umepita na mtoto hajulikani kama yuko salama na yuko na nani hivyo  alikuwa anaomba serikali ilishughulikie suala hiyo ili kujua hatima ya mtoto huyo.

 

Picha ya mlalamikaji wa kudai kunyanganywa mtotyo wa miezi mitatu(3)na baba asiyetambulika na familia ya

 WEBSITE DESIGN AND DEVELOPMENT IN TANZANIA

Website is one of the methods people use to advertise their business, talents and explore opportunities around the world. It can take you some days or months to learn about website design and development. 

At Anzanait,  we provide people with skills to learn how design and develop website. It is not difficult as most of people think, but it needs one's time and commitment to learn about it

Today we are going to look at different types of websites;

Static websites; these are website with which once developed by a your developer or you it's contents does not change. It will remain with the content you put in it until you change it manually.

The second type of website is dynamic websites. These are good and more flexible in terms of content. Its contents changes with time as people enter their contents. For more information about website design and development and website services please don't hesitate to call us from +255765970455, / +255788968945